“Ingawa uhalisia wenu unaathiriwa na utofauti mpana wa hali, hata hivyo shauku ya kuleta mabadiliko yenye manufaa na uwezo wa huduma yenye maana, vyote viwili vikiwa ni sifa bainifu za hatua yenu katika maisha, havina mipaka kwa mbari yoyote au utaifa, na wala havitegemei mali za kimwili. Kipindi hiki kiangavu cha ujana mkipitiacho hupitiwa na wote—lakini ni kifupi na hurushwa upande mmoja hadi mwingine na shawishi nyingi za kijamii. Ni wa umuhimu ulioje, basi, kujitahidi kuwa miongoni mwa wale ambao, katika maneno ya ‘Abdu’l-Bahá, `wamechuma tunda la Maisha’.”
— Nyumba ya Haki ya Ulimwengu
Vijana wametekeleza nafasi ya msingi sana katika historia ya Kibahá’í. Báb Mwenyewe alitangaza utume Wake alipokuwa na umri wa miaka ishirini-na-tano tu na wengi wao kati ya kundi la wafuasi Wake walikuwa katika mwanzo wa ujana wao walipoukumbatia Ufunuo Wake. Wakati wa kipindi cha Bahá’u’lláh na ‘Abdu’l-Bahá , vijana walikuwa kwenye safu ya mbele ya jitihada za kutangaza Imani mpya na kushiriki mafundisho yake na wengine.
Wakifuata njia ambayo watu hawa na wengine wa kipekee walifungua, maelfu ya vijana Wabahá’í wameinuka katika kila kizazi kuitikia mwito wa Bahá’u’lláh. Jitihada zao huongozwa na Asasi Kuu ya Imani ya Kibahá’í—leo, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu—ambayo inawahamasisha vijana kuchota kutoka ari na bidii ambazo ni tabia za kipindi cha ujana na hivyo kutoa michango yenye uamuzi kwenye uendelezaji mbele wa ustaarabu wa kiroho na kimwili.
Wigo wa mwongozo na uhamasisho unaotolewa na Nyumba ya Haki na wa mwitikio wa vijana Wabahá’í leo ni mpana sana, na shughuli zinazosababishwa nao ni anuwai mno, kiasi kwamba haziwezi kuelezwa kwa jumla hapa. Kurasa za mkusanyiko wa mada hii, basi, hutia mkazo kwenye mfano mmoja: mfululizo wa makongamano ya vijana katika maeneo 114 kote ulimwenguni ambayo yaliendeshwa mwaka 2013 pamoja na mawimbi ya mikusanyiko midogo zaidi inayoendelea kufanyika tangu wakati huo.
Unaweza kusoma ujumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu uliopelekwa kwa makumi elfu ya vijana washiriki, kuangalia mfululizo wa filamu fupi kwa jina “Kuhudumia Binadamu”, na kuona taarifa kutoka kila moja ya mikusanyiko hii ya 2013 katika sehemu maalum ya tovuti ya Idara ya Habari za Ulimwengu za Kibahá’í.